Bunge la India linajadili rushwa

Bunge la India linajadili mswada wa kupambana na rushwa, ili kumshawishi mwanaharakati anayepiga vita ufisadi, aache kususia chakula.

Haki miliki ya picha AP

Mwanaharakati huyo, Anna Hazare, amekataa kula kwa siku 12 sasa, na madaktari wanasema wana wasiwasi mkubwa ju ya afya yake.

Bwana Hazare, mwenye umri wa miaka 74, ameungwa mkono na wananchi wa India waliochoka na rushwa kubwa.

Akifungua mjadala ambao utakuwa wa kihistoria, waziri mmoja wa chama tawala, Pranab Mukherjee, alisema India iko njia panda; na macho yako juu ya demokrasi ya bunge.

Alimsihi Anna Hazare aache kususia chakula; na kwamba ingawa Bwana Hazare anaungwa mkono juu ya sheria aliyopendekeza ya kupambana na rushwa, hata hivo lazima kupatikane suluhu itayoruhusiwa na katiba ya India.

Madaktari wanaomshughulikia Bwana Hazare, wanasema hali yake inazidi kuwa mbaya haraka.

Lakini mwanaharakati huyo amesema hatomaliza funga yake, hadi bunge litapopiga kura na kupitisha sheria yake.