Maporomoko Uganda yaua watu Bulambuli

Image caption Maporomoko yatokea tena baada ya yaliyotokea mwaka 2010

Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wanasema.

Wakazi wanahofu kuwa 35 huenda wamekufa katika wilaya ya Bulambuli lakini mpaka sasa miili 24 imepatikana.

Mwaka uliopita mamia walikufa katika tukio kama hilo katika miteremko ya Mlima Elgon.

Maafisa wanasema watawahamisha hadi nusu milioni ya watu kuepuka hali hiyo kujitokeza tena.

Waliokufa Bulambuli, kilometa 270 (maili 167) kaskazini mashariki mwa Kampala, wanatokea kwenye vijiji viwili, mseamji wa Shirika la Msalaba Mwekundu Catherine Ntabadde ameliambia shirika la habari la AFP..

Amesema watu wawili wameokolewa.

Kufuatia janga la Mlima Elgon, imearifiwa kuwa ongezeko la watu la haraka limesababisha kukatwa kwa miti kwenye milima na kufanya maporomoko na mafuriko kutokea mara kwa mara.