Stoke wamtaka Lukaku wa Chelsea kwa mkopo

Klabu ya Stoke have imeikabili Chelsea ikikusudia kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Romelu Lukaku.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Romelu Lukaku

Lukaku, mwenye umri wa miaka 18, aliwasili Stamford Bridge mapema mwezi wa Agosti na alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi akiwa na Chelsea siku ya Jumamosi walipoishinda Norwich mabao 3-1.

Wakati huo huo Stoke wamo mbioni kumsajili Wilson Palacios kutoka Tottenham kwa kitita cha paundi milioni 6 na kiungo huyo anajiandaa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Stoke katika siku za karibuni pia imehusishwa kutaka kumchukua mshambuliaji wa Spurs Peter Crouch.

Na vyombo vya habari vya Denmark vimesema mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner huenda yupo njiani kujiunga na Stoke.

Chelsea ilimsajili Lukaku kwa kitita cha paundi milioni 20 tarehe 6 mwezi wa Agosti. Ni mchezaji mashuhuri nchini Ubelgiji baada ya kuwa mfungaji bora katika ligi ya nchi hiyo msimu wa 2009-2010 alipokuwa na umri wa miaka 16.

Alifunga mabao 16 katika mechi 37 za ligi msimu uliopita na akafunga bao lake la kwanza katika mechi ya kimataifa Ubelgiji ilipoilaza Urusi mabao 2-0 mwezi wa Novemba.