Waasi Libya wakataa jeshi la amani la UN

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wananchi wa Libya wakisherehekea Eid mjini Tripoli

Uongozi wa mpito nchini Libya umekataa wazo la kuweka jeshi lolote la kimataifa aina yoyote ya jeshi la kimataifa, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya amesema.

Ian Martin amesema Umoja wa Mataifa ulifikiria kupeleka waangalizi wa kijeshi nchini humo.

Taarifa hizo zimekuja wakati wapiganaji wanaolitii Baraza la Mpito wakikaribia ngome ya Gaddafi ya Sirte kutokea mashariki na magharibi.

Wamepewa hadi Jumamosi kusalimu amri.

Hata hivyo msemaji wa Kanali Gaddafi aliyekimbia Moussa Ibrahim, amekataa amekataa kukubaliana na kusalimu amri, Shirika la habari la AP linaripoti.

"Hakuna taifa lenye heshma yake litakubali kutii makataa kutoka kwa genge lenye silaha," alisema kwa njia ya simu alipozungumza Jumatatu usiku na AP.

Bw Ibrahim alirejea ahadi ya Kanali Gaddafi ya kumtuma mwanawe Saadi kufanya majadiliano na waasi na kuunda serikali ya mpito, shirika hilo la habari limesema.

Mwakilishi msaidizi wa Libya katika Umoja wa Mataifa Ibrahim Dabbashi, ameiambia BBC kwamba hali ya Libya ilikuwa ya kipekee

"Umoja wa Mataifa unaangalia uwezekano wa kuweka wanajeshi wa kulinda amani nchini humo lakini mgogoro wa Libya ni suala maalum.

"Si vita vya wenyewe kwa wenye, si mzozo kati ya vyama, ni watu ndio wanaojilinda wenyewe dhidi ya udikteta."

Hata hivyo, Bw Martin alisema Umoja Wa Mataifa unatarajia kuombwa kusaidia kuimarisha jeshi la polisi"

Kwa sasa hatutarajii kuomba jeshi la kulinda amani," alisema baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

"Ni wazi kuwa walibya wanataka kuepuka aina yoyote ya jeshi kuletwa na Umoja wa Mataifa au yeyote," alisema.

Bw Martin aliongeza kuwa changamoto kubwa kwa Umoja wa Mataifa kuisaidia nchi kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia.