Watu wanakimbia Blue Nile, Sudan

Maelfu ya watu wa Sudan wanakimbia mashambulio ya jeshi la serikali dhidi ya wapiganaji kwenye majimbo mawili yaliyo kaskazini ya mpaka wa Sudan Kusini.

Haki miliki ya picha Reuters

Umoja wa Mataifa unasema watu elfu 16 kutoka jimbo la Blue Nile, wamekimbilia Ethiopia.

Na 3000 wamekimbia makwao katika jimbo al Kordofan Kusini.

Wadadisi wanasema serikali mjini Khartoum inajaribu kuwazima wapiganaji katika majimbo yote mawili kabla hawajaanza kupata nguvu na kutaka kujitenga.