Kesi ya Ingabire kuanza leo mjini Kigali

Nchini Rwanda kesi ya mwanasiasa wa upinzani Bi Ingabire Victoire inatarajiwa kuanza siku ya Jumatatu mjini Kigali, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.

Image caption Ingabire Victoire

Bi Victoire Ingabire anazuiliwa tangu mwezi October mwaka uliopita kwa mashtaka ya kukana mauaji ya kimbari, uhaini na kushirikiana na makundi ya kigaidi likiwemo kundi la waasi wa FDLR.

Bi Victoire Ingabire aekanusha mashtaka hayo akisema yamepangwa kisiasa.