Mazungumzo ya Somalia yafanywa Mogadishu

Mkutano umeanza mjini Mogadishu, Somalia, kutafuta ufumbuzi wa kisiasa nchini humo.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Lengo ni kufanya uchaguzi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Somalia haikupata serikali madhubuti tangu mwaka wa 1991, na imeongozwa na tawala za mpito kwa miaka saba sasa.

Makundi ya kisiasa ya Somalia na viongozi wa majimbo wanahudhuria.

Lakini makundi muhimu, kama la wapiganaji wa Kiislamu, la al-Shabaab, na wawakilishi wa eneo lilojitenga la Somaliland, hawamo katika mazungumzo hayo.