Bolt awaongoza wenzake kuvunja rekodi

Usain Bolt ameiongoza Jamaica kuweka rekodi mpya ya dunia ya sekunde 37.04 wakati waliposhinda mbio za mita 4x100 kwa wanaume kupokezana vijiti wakati wa siku ya mwisho ya mashindano ya riadha ya Dunia mjini Daegu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Usain Bolt

Timu hiyo ya Jamaica, iliyojumuisha pia bingwa mpya wa dunia wa mbio za mita 100 Yohan Blake, iliishinda timu ya Ufaransa na St Kitts and Nevis.

Timu ya Marekani ilishindwa kumaliza baada ya mkimbiaji wake mmoja kuanguka baada ya kugongana na mkimbiaji wa Uingereza, ambaye alikiangusha kijiti wakati wa kumkabidhi mwenzake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maria Savinova

Naye Mariya Savinova wa Urusi naye alimaliza vizuri na kumshinda Caster Semenya wa Afrika Kusini katika fainali ya mbio za mita 800 wanawake.