Walimu wagoma Afrika Mashariki

shule ya msingi

Walimu wa DRC, Kenya na Uganda wanaendelea na migomo wakitaka masharti mbalimbali yatekelezwe na Serikali zao ili waendelee kazini.

Chama cha walimu nchini Kenya kinataka zaidi ya walimu 28,000 waajiriwe ili kupunguza upungufu wa walimu katika shule za umma za msingi na upili. Mashauriano kati ya walimu hao na Waziri Mkuu Raila Odinga yalivunjika jana na walimu wakaapa kuendelea na ShHuku shule zikitarajiwa kufunguliwaa hii leo kwa muhula wa tatu wa mwaka nchini Kenya chama cha walimu nchini kimeapa kuanza mgomo wake baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati ya chama hicho na serikali.

"walimu kwa wakati huu hawataki mishahara mikubwa bali wanataka tu walimu wengine waajiriwe ili kazi shuleni iwe ya hali ya juu," mwenyekiti wa Kitaifa wa chama kikuu cha walimu nchini Kenya (KNUT), Wilson Sossion Chama alisema.

Wakati huohuo migomo mingine ya walimu inaendelea DRC na Uganda. Katika mataifa haya mawili walimu wanataka kuongezewa mishahara na kuimarishwa kwa hali yao ya kazi.