Mahabusu 1000 watoroka gerezani DRC.

Zaidi ya mahabusu 1,000 wametoroka gereza moja kubwa DRC Congo baada ya watu wenye bunduki waliofunika nyuso zao kuvamia gereza hilo.

Image caption Wapiganaji wa Mai Mai

Miongoni mwa waliotoroka gerezani ni kiongozi mmoja wa kundi la wapiganaji wa Mai Mai aliyekuwa amehukumiwa kifo

Gédéon Kyungu Mutanga.

Tukio hilo ni la kutisha nchini kwa sababu umesalia muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.

Maafisa wa Mkoa wa Mashariki mwa Katanga walisema watu wanane waliingia katika gereza hilo wakijisingizia kuwa wageni wa wafungwa kabla ya kuvamia gereza hilo na kumkomboa kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Mai Mai ajulikanaye kama "kamanda Gedion".

"Watu hao walifyatulia risasi polisi na walinzi katika gereza hilo na kuwaua wawili kati yao," Waziri wa Maswala ya ndani wa Jimbo la Katanga, Dikanga Kazadi, alisema.

"Walimkomboa kiongozi huyo wa zamani wa wapiganaji wa wafungwa wengine 967, na kufikia sasa 150 kati yao wamekamatwa na kurejeshwa gerezani," Kazadi aliongezea.

Ingawa walioshuhudia kisa hicho walisema waliona zaidi ya maiti mbili hakuna aliyeweza kuthibitisha madai hayo.

Ripoti za hivi karibuni zinasema wafungwa 152 waloikuwa wametoroka wamekamatwa na polisi.

Baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitalini moja mjini Kisingani.

Hata hivyo kiongozi wa zamani wa kundi wa waasi la Mai Mai Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye alikuwa miongoni mwa wafungwa hao waliotoroka, hajulikani aliko.