Rais Bashir atangaza M'Darfur makamu

Rais wa Sudan amemtangaza mwanasiasa kutoka Jimbo la Darfur, Adam Youssef kama Makamu wake wa Rais, kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo Suna.

Habari hizo ni kufuatia pia mojapo ya nafasi mbili za Makamu wa Rais kubaki bila mtu baada ya sehemu ya kusini kujitenga na hivyo kupatikana kwa Taifa jipya la Sudan ya kusini.

Bw. Youssef ni kutoka katika mojapo ya makabila ya waarabu asilia wa Darfur na ni hivi karibuni ndipo kajiunga na chama cha Bw. Omar al-Bashir.

Bw.Bashir amekanusha tuhuma za kusababisha vitendo vya uhalifu katika eneo la magharibi mwa jimbo la Darfur.

Image caption Njama ya kuimarisha Uarabu Darfur

Umoja wa Mataifa unasema kuwa hadi watu laki tatu (300,000 wamefariki kutokana na mzozo ulioendelea kwa kipindi cha miaka minane baina ya makundi ya waasi wenye asili za kiafrika na wapiganaji wenye asili ya kiarabu walioko huko Darfur.

Serikali ya Sudan inakanusha na kusema kua idadi hiyo imezidishwa na kuongezea kua takwimu za ukweli ni watu 12,000 waliopoteza maisha yao.

'hawaoni tofauti' Baadhi ya makundi ya waasi huko Darfur yamepinga kumtangaza Bw.Youssef na kutaja uwamuzi huo kama ishara tu.

Makundi yamesema kuwa uteuzi huo ni sehemu ya njama ya kuimarisha uarabu huko Darfur. Hatoleta mabadiliko yoyote, alisema afisa mwandamizi katika vuguvugu linalowania sheria na usawa(JEM) kwa kifupi, el Tahir el -Faki.

Image caption Kambi ya wakimbizi wa ndani

Kundi hilo la JEM pamoja na jingine la Sudan Liberation Army yamepinga mpango wa hivi karibuni kati ya serikali kuu ya Sudan na LJM au Liberation and Justice Movement, kundi ambalo ni unganishi la mpasuko wa makundi hayo mawili.

Bw.Youssef alikua kiongozi shupavu mwenye msimamo mkali wa Kiislamu katika chama cha upinzani cha Popular Congress Party hadi mwei novemba mwazka 2010.

Mahakama ya Kimataifa kuhusu jinai imetoa waranti za kutaka Bw.Bashir akamatwe pamoja na maofisa wake kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji ya kimbari pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu huko Dafur.