Idadi ya wamarekani maskini yaongezeka.

Barak Obama
Image caption Rais wa Marekani Barak Obama

Idadi ya raia wa Marekani wanaoishi katika umaskini imeongezeka hadi watu milioni 46.2 mwaka uliopita,kwa mujibu wa idara ya kuhesabu watu Marekani,karibu mtu mmoja kati ya raia sita,wanaishi katika hali hiyo.

Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa umaskini umeongezeka hadi asilimia 15.1%,kutoka 14.3% mwaka 2009.Idadi ya raia wa Marekani wasio na bima ya afya pia imepanda hadi milioni 49.9.

Kiwango cha umaskini kimeongezeka kwa mfululizo

Kiwango hiki cha umaskini ndicho cha juu zaidi tangu mwaka 1983,na ni sawa ya mwaka 1993.

Idadi ya raia wa Marekani wanaoishi katika hali ya umaskini sasa imeongezeka kwa miaka minne mfululizo.

Wamarekani weusi na wenye asili ya uhispania waathirika zaidi

Tafsiri ya umaskini nchini Marekani ni kuwa na kipato cha dola $22,314 kila mwaka,au chini yake kwa familia ya watu wanne,na dola $11,139 kwa mtu mmoja.

Idara hiyo ya kuhesabu watu pia imeonyesha kuwa umaskini miongoni mwa raia wa Marekani weusi na wenye asili ya kihispania iko juu zaidi katika mwaka uliopita-asilimia 27.4% na 26.6% mtawalia.