Mwandishi habari aikimbia Ethiopia

Mwandishi kutoka Ethiopia, Argaw Ashine ameiambia BBC kuwa ameikimbia nchi yake kufuatia nyaraka za Wikileaks zilizochapishwa kuhusiana na mawasiliano ya kibalozi za Marekani mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyaraka za Wikileaks

Amesema kuwa alihojiwa na maofisa waliotaka aelezee vyanzo vya taarifa zake katika nyaraka za mwaka 2009 alipodai kuwa wandishi habari walinyanyaswa.

Hata hivyo Wikileaks limekanusha kua lilimnukuu Bw.Argaw kama kachero wa Balozi za Marekani na hakuna mwandishi wa habari aliyetajwa".

Lakini Kamati ya kulinda wandishi wa habari (CPJ)inasema kuwa hii ni mara ya kwanza ambapo mwandishi wa habari amehusishwa na nyaraka za Wikileaks.

Kamati hiyo imesema kuwa"Hofu yetu ya kutaka kuepuka athari kufuatia ufichuzi wa nyaraka za Wikileaks na sasa hofu yetu imetimia, alisema mkurugenzi mtendaji wa Kamati hiyo yenye makao yake nchini Marekani.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia Shimellis Kemal ameiambia BBC kuwa sheria za nchi yake zinawalinda wandishi wa habari katika kuficha vyanzo vya habari zao".

Bw Argaw, ambaye ni mwandishi wa gazeti la Daily Nation nchini Kenya pia ni mwenyekiti wa Shirikisho la wandishi wa habari wanaoandika habari kuhusu mazingira, na alitaka mahali alipo pasifichuliwe kwa sababu za usalama.

Amesema kuwa alitoroka mwishoni mwa juma lililopita alipotakiwa afike mbele ya vyombo vya dola.