Wazee wanyan'ganywa mtoto kwa umri

Wazazi wa mtoto mchanga akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi minne wamenyanganywa mtoto huyo na kutaka apewe wazazi wengine kwa sababu wazazi hao wana umri mkubwa kupindukia, huo ni uwamuzi wa koti moja ya mji wa Turin nchini Italia.

Mama mtoto ana umri wa miaka 57 huku baba ana umri wa miaka 70. Kesi hii imezusha hisia za kukemewa katika vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Wazazi hao Gabriella na Luigi Deambrosis wanaishi katika mji mdogo ulio kwenye bonde la milima ya Alps. Waliofunga ndoa yao miaka 20 iliyopita. Tangu hapo juhudi zao za kupata mtoto hazikufanikiwa, na kila walipojaribu kuomba ruhsa ya kuasili mtoto walikataliwa kwa misingi ya kuwa wenye umri mkubwa.

Kutokana na juhudi zao kukwamishwa na mfumo wa nchi yao waliamua kwenda nchi za nje ili waweze kupanga uzazi. Mwezi mmoja baada ya kujifungua mtoto mwaka jana mjini Turin majirani wakatoa taarifa kuwa wazazi hao walimuacha mtoto yule ndani ya gari kwa mda mfupi.

Kufuatia taarifa hiyo, kotio ikaamuru polisi wawanyanganye wazazi mtoto na akabidhiwe wazazi wa kupanga.

Wazee hao wameruhusiwa kumuona mtoto wao mara moja katika kipindi cha majuma mawili tangu wakati huo.

Hivi sasa koti ya vijana imeamuru kuwa lazima mtoto huyo atolewe kwa ajili ya kuasiliwa na wazazi wenye umri mdogo kwa misingi ya kwamba 'mtoto huyo ni matunda ya uzazi wa njia isiyostahiki kimaumbile ukiwezeshwa kwa njia ya sayansi.

Wazazi hao hawakuwahi kutafakari kuwa binti yao angekabiliwa na shida ya kuwa yatima mapema hivi.

Mama mtoto alikuwa na umri wa miaka 36 wakati wa kuolewa na alijitahidi kwa mda mrefu kupata uzazi kwa njia za kawaida.

Wazazi hao wanajitahidi kukata rufaa ya uwamuzi wa koti wa kunyanganywa mtoto wao, wakitaka waruhusiwe chini ya sheria ya hivi karibuni nchini Italia inayokubali tiba ya uzazi na mimba za kupandikiza,ingawa sheria hiyo imeshutumiwa na vyombo vya habari.

Kura ya maoni iliyoitishwa mwaka 2004 kubadili sheria hiyo ilishindwa kupata idadi iliyohitajika baada ya Vatican kuingilia kati kwa kuwataka wafuasi Wakatoliki wasishiriki kura hiyo.