Wasifu wa Bw Michael Sata

Rais mtarajiwa wa Zambia Michael Sata anatambulika zaidi kwa jina la utani King Cobra.

Alipewa jina hilo kwa kuwa na mazoea ya kutoa kauli nzito ambazo zimewavutia sana watu wenye kipato kidogo na vijana wengi nchini humo.

Baada ya kugombea urais mara nne, hatimae kiongozi huyu mahiri wa upinzani mwenye umri wa miaka 74 anaingia Ikulu.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bw Michael Sata

Anasema chini ya siku 90 atasambaza utajiri wa nchi hiyo unaotokana na madini ya shaba kote nchini.

Wadadisi wa siasa wanasema ushindi wake umechangiwa na hasira watu walionayo kuhusu serikali kuzembea katika kukabili rushwa na umasikini uliokithri.

Michael Sata, kwa kipindi fulani alikuwa akifagia kituo cha treni cha Victoria mjini London lakini baada ya kurudi nyumbani, alihudumu katika ngazi mbali mbali serikalini ambapo alisifika kwa utendaji kazi wake na uadilifu.

Mwaka 2001 alijiuzulu kutoka chama tawala MMD na kuunda chama chake cha Patriotic Front .

Bw Sata sio mgeni kwa kuzua ugomvi hasa kauli zake za kuwatisha wawekezaji kutoka China ambao wakati fulani alisema wanawanyonya tu Wazambia.

Bila shaka kufuatia ushindi huu watafuatilia sera zake kwa karibu.

Wakosaji wake pia wanasema ana dalili za kuwa kiongozi wa kiimla lakini katika kampeni zake ambapo nembo yake ilikuwa safina sawa na ya nuhu.

Alionyesha kubadilisha misimamo yake mikali.

Alipoulizwa kwanini anagombea tena urais safari hii, alisema bila kuwa kung'ang'ania basi huwezi kufaulu kwa chochote.

Sasa anaingia kwenye kipindi kingine cha utakelezaji je ataleta mabadiliko?