Abbas ashangiliwa Palestina

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amepokelewa kama shujaa, aliporudi nyumbani kutoka Umoja wa Mataifa, ambako aliomba eneo la WaPalestina kuwa mwanachama kamili.

Haki miliki ya picha AP

Bwana Abbas aliuambia umati uliomshangilia mjini Ramallah, kwamba hawatoshiriki kwenye mazungumzo na Israil, ikiwa hawatotambuliwa kimataifa, na Israil haikuacha kujenga makaazi katika Ufukwe wa Magharibi.