Mabomu mane yaripuka Kerbala, Iraq

Mabomu mane yameripuka katika mji wa Kerbala, Iraq, na kuuwa watu 10, na kuwajeruhi wengine kadha.

Wakuu wa jeshi walisema maafisa wane ni kati ya wale waliokufa katika shambulio hilo, ambalo wanasema limefanywa na Al Qaeda.

Bomu moja liliripuka nje ya ofisi ya serikali mjini humo, mji ulioko kilomita mia moja kusini ya Baghdad.

Ghasia zimeongezeka nchini Iraq katika majuma ya karibuni.