Waasi wa Libya waingia wa Sirte

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa Libya wafanikiwa kuingia Sirte

Wapiganaji wanaompinga Kanali Gaddafi wamefanikiwa kuingia mji alikozaliwa Gaddafi wa Sirte kutokea mashariki mwa mji kwa mara ya kwanza, huku wakiendelea na mashambulizi.

Askari hao walipigana kwa makombora na wanajeshi wanaomtii Kanali Gaddafi kupitia viunga vya mji huo.

Hatua hiyo imekuja siku mbili baada ya askari wa Baraza la Mpito NTC walishambulia kutokea magharibi kabla ya kurudi nyuma.

Sirte ni moja ya ngome za Kanali Gaddafi zilizobakia.

Mwandishi wa BBC Alastair Leithead, akiwa mjini Sirte, anasema raia wamekuwa wakikimbia mji huo baadhi wakiwa hawajui kuwa Tripoli ilishaanguka

Wengi wao waliogopa, anasema, baada ya kuambiwa kuwa wapiganaji wa waasi watachinja makoo yao iwapo wataonekana mjini humo.

Mwandishi wa BBC anasema raia waliobakia wako katika hatari wakiwa wamenaswa katikati ya mapigano makali.

Wanaomtii Gaddafi wamekuwa wakiulinda mji huo kutokana na mashambulizi ya NTC katika wiki za karibuni.

Vikosi vya NTC vililazimika kurudi nyuma siku ya Jumamosi baada ya kukaribia katikati ya mji wakitokea magharibi.

Sirte ni mji unaokua mapigano mengi yanafanyika kutokea mbali kwa kutumia makombora na vifaru pamoja na mashambulizi ya anga ya NATO.

Sirte na Bani Walid, kiasi cha kilometa 250 (maili 155) magharibi zaidi ni miji pekee mikubwa ambayo bado ina misimo kinyume na NTC.

Mapigano yanaendelea kuzunguka mji wa Bani Walid, huku kamanda mmoja wa akiimbia shirika la habari la AFP kuwa anatajia mapigano ya mwisho ya udhibiti yanaweza kuwa ndani ya siku mbili zijazo.

"Tangu asubuhi tumekuwa tukivipiga vikosi vya Gaddafi mfululizo kw makombora, vifaru na silaha nyingine za angani," Kamanda Mohamed al-Seddiq ameliambia shirika la habari.

"Tunapambana na mapambano makali ndio maana tunatumia silaha nzito na hatutapeleka askari wa miguu kwa sasa."

Baraza la NTC halijafanikiwa kujua aliko Kanali Gaddafi, aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 40.

Lakini baadhi ya watoto wake na baadhi ya watu wake wa karibu wamekimbilia uhamishoni.