Mapigano makali kwenye ngome za Gaddafi

Kumekuwa na mapigano makali katika mji wa Sirte nchini Libya, ambapo majeshi yanayounga mkono baraza la mpito yakikumbana na uzito mkubwa na wanaomtii Gaddafi.

Mwandishi wa BBC aliye nje ya mji huo alisema pande hizo mbili zimekuwa zikifyatuliana risasi, roketi na makombora.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sirte, Libya

Maelfu ya raia wamebaki Sirte, mashariki mwa mji, Tripoli.

Mashirika ya kuhudumia binadamu yameonyesha wasiwasi juu ya hali za raia wanazokabiliana nazo.

Sirte inabaki kuwa moja ya ngome zilizobaki zenye wale wanaomwuunga mkono Kanali Gaddafi, na mji wa Bani Walid kilomita 250 kutoka magharibi mji mwengine pekee unaoshikiliwa.