Taifa Stars yataja kikosi chake

Tanzania Haki miliki ya picha Online
Image caption Taifa Stars

Tanzania imetangaza kikosi kitakachopambana na Morrocco katika michuano ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.

Taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Tanzania TFF imesema Taifa Stars ambayo inafundshwa na Jan Poulsen itaondoka Oktoba 6 kwenda Morrocco, na kujitupa uwanjani Oktoba 9 mjini Marrakech.

Kikosi hicho cha wachezaji 23 ni:

Makipa:

Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars) Juma Kaseja (Simba) Shabani Kado (Yanga)

Mabeki:

Shadrack Nsajigwa (Yanga) Erasto Nyoni (Azam) Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) Amir Maftah (Simba) Aggrey Morris (Azam) Juma Nyoso (Simba) Victor Costa (Simba)

Viungo:

Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway) Nurdin Bakari (Yanga) Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) Jabir Aziz (Azam) Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) Mrisho Ngassa (Azam) Ramadhan Chombo (Azam)

Washambuliaji:

Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam) Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) John Bocco (Azam) Hussein Javu (Mtibwa Sugar)

Tanzania iko kundi D, pamoja na Algeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Morrocco.

Tanzania ina pointi 5 baada ya michezo mitano na kushinda mmoja, sawa na Algeria. Morrocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaongoza kundi hilo zikiwa na pointi 8.