Kampeni za uchaguzi zaanza Tunisia

Kampeni zimeanza nchini Tunisia, za uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi -- ambao unafuatia mapinduzi ya mwezi Januari, yaliyomtoa Rais Zine El Abidine Ben Ali, ambaye aliondoka baada ya maandamno ya fujo.

Haki miliki ya picha Getty

Wapigaji kura watachagua wawakilishi wao katika bunge ambalo litakuwa na mwaka wa kutayarisha katiba mpya, kabla ya uchaguzi mwengine kufanywa.

Wawakilishi kama elfu-10 wa vyama 80 vya kisiasa wanashiriki katika uchaguzi huo.

Uchaguzi utafanywa tarehe 23 mwezi huu.