Zardari ataka zungumza na Marekani

Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan, ametoa wito kwa Marekani kuanza tena mazungumzo ya maana na nchi yake.

Haki miliki ya picha AFP

Katika makala aliyoandika katika gazeti la Jumamosi la Washington Post la Marekani, Rais Zardari alisema Marekani inahitaji kuzungumza na Pakistan, badala ya kuiambia maneno tu.

Matamshi hayo yanakuja baada ya afisa mkuu wa jeshi la Marekani, Adimeri Mike Mullen, kuishutumu Pakistan kuwa inawasaidia wapiganaji.

Rais Zardari amekanusha vikali shutuma hizo, na kusema kuwa wapiganaji hao, ambao Marekani inashutumu wanasaidiwa na Pakistan, wameuwa raia zaidi ya elfu-30 wa Pakistan.