Tantawi anamtetea Mubarak

Mkuu wa serikali ya mpito ya kijeshi ya Misri amesema rais aliyetolewa madarakani, Hosni Mubarak, hakupata kuomba jeshi liwapige risasi waandamanaji.

Haki miliki ya picha Reuters

Akizungumza katika ufunguzi wa mradi mpya wa karakana kusini ya Cairo, Field Marshal Hussein Tantawi alisema alitoa ushahidi mbele ya Mungu na alisema kweli.

Kiongozi huyo alitoa ushahidi katika kesi ya Bwana Mubarak, kwenye kikao cha siri, juma lilopita.

Alikuwa waziri wa ulinzi wa Bwana Mubarak - na ushahidi wake ulionekana kuwa muhimu katika kesi hiyo, ambapo Rais Mubarak anakabili mashtaka ya kutoa amri kwa askari kuwapiga risasi waandamanaji.