Walibya wanahama Sirte

Maelfu ya Walibya wametumia nafasi waliyopata kwa sababu ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda, kuukimbia mji wa Sirte -- moja kati ya ngome za wapiganaji wa Kanali Gaddafi.

Haki miliki ya picha AFP

Mwandishi wa BBC katika kitongoje cha Sirte anasema ameona mtiririko wa familia zikiuhama mji kwa magari yaliyojaa mizigo pomoni.

Wengi wakionesha khofu na shida.

Wapiganaji wa serikali mpya ya mpito ya Libya, wameuzingira mji wa Sirte kwa majuma kadha, ili kujaribu kuwatoa wafuasi wa Kanali Gaddafi wanaopigana, lakini wapiganaji wamepata upinzani mkubwa.

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu linasema hali ya wakaazi wa mji huo ni mbaya sana