Upigaji kura umemalizika Igunga

Wananchi wa Tanzania katika jimbo la Igunga, katikati mwa nchi, wamemaliza kupiga kura.

Inakisiwa kuwa nusu wa wapigaji kura wamejitokeza, karibu sawa na wakati wa uchaguzi mkuu.

Kiti hicho kilichoachwa wazi na Mbunge Rostam Aziz wa chama tawala cha CCM, kimeona mashindano hasa kati ya vyama vitatu vikubwa - CCM, CHADEMA na CUF.

Wakuu wa uchaguzi wanakisia kuwa matokeo huenda yakawa tayari leo, Jumapili usiku.