Mkuu wa majeshi amtetea Mubarak

Mkuu wa majeshi wa Misri Field Marshal Tantawi alisema aliyekuwa rais Hosni Mubarak hakuwahi kuwaambia wanajeshi kuwapiga risasi wanaharakati wakati wa machafuko mapema mwaka huu.

Matamshi hayo, yaliyotolewa wakati wa sherehe kusini mwa mji mkuu huo, wiki moja baada ya Field Marshal Tantawi kutoa ushahidi kwa siri katika kesi ya Bw Mubarak.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Field Marshal Tantawi

Bw Mubarak anashtakiwa kwa kuua waandamanaji wakati wa uasi wa siku 18 iliyomlazimu kuondoka madarakani.

Takriban waandamanaji 850 waliuawa.

Field Marshal Tantawi, aliyekuwa waziri wa ulinzi chini ya Bw Mubarak kwa miaka 20 alisema, "Majeshi yanapigana kwa ajili ya Misri na si kwa ajili ya mtu yeyote tu, yoyote atakayekuwa."

Alisema, "nilitoa ushahidi mbele ya Mungu na nimesema ukweli."