Maisha jela kwa maharamia wa kisomali

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uharamia umeshamiri katika bahari Hindi

Raia wawili wa Somali wamehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani kwa kuhusika na utekaji nyara mbaya wa mashua ya kifahari mwezi wa pili mwaka huu.

Muhidin Salad Omar na Mahdi Jama Mohamed walihukumiwa katika mahakama ya jimbo la Norfolk, Virginia. Tukio hilo la utekaji nyara lilisababisha mauaji ya raia wanne wa Marekani.

Walikuwa miongoni mwa genge la watu 19 walioteka nyara mashua kusini mwa Oman,wakitarajia kupata kikombozi kwa abiria.

Wengine zaidi watahukumiwa siku ya Jumanne.

Washirika wawili wa Omar walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwezi wa nane. Watatu wengine wanashutumiwa kwa mauaji na huenda wakahukumiwa kifo.