Marekani na Nato hawajafikia malengo Afghanistan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majeshi ya Marekani huko Afghanistan

Baada ya miaka 10 nchini Afghanistan, Marekani bado haina mbinu ya kumaliza mzozo huo, haya ni kwa mjibu wa Jenerali mstaafu Stanley McChrystal.

Jenerali McChrystal amesema kuwa Marekani na washirika wake wa Nato bado hawajakamilisha malengo yao.

Harakati hizo zililenga kumsaka Osama Bin Laden baada ya shambulio la 9/11 na kuangamiza Taliban.

Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya raia 10,000 wamefariki dunia kutokana na mapigano hayo katika muda wa miaka mitano iliyopita.

Zaidi ya wanajeshi 2,500 wa kimataifa wameuawa - wengi wao wakiwa wamarekani.

Mapigano hayo tayari yameshinda vita vya Vietnam na kwa sasa ni vita vya muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani.