Msaada wafika Kismayo

Shirika la msalaba mwekundu nchini Somalia, limefikisha chakula cha msaada kwa mara ya kwanza, kusini kwa bandari ya Kismayo, ambayo iko chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa al-shabaab.

Mwandishi wa BBC nchini Somalia alisema msafara wa malori 15 uliwasili katika mji huo.

Ni moja ya shughuli kubwa zilizoanzishwa juma hili, kutoa chakula kwa zaidi ya watu milioni moja, wanaoathirika na ukame kusini mwa nchi hiyo.

Shirika hilo limesema shughuli hiyo ilianza, kufuatia mazungumzo magumu na kundi la al-shabaab.

Limedokeza kuwa litagawa mbegu na mbolea kwa kama wakulima laki mbili unusu.