Sebastien Vettel ajiandika

Dereva wa Timu ya magari ya Red Bull, Sebastian Vettel amehitimisha msimu wa mwaka 2011 kwa ushindi wa taji la mbio za magari ya langalanga licha ya dereva wa Timu ya magari ya McLaren Jenson Button kushinda mbio za Japan mapema leo.

Haki miliki ya picha Getty

Lau kama Button angeshinda na Sebastien Vettel amalize nje ya nafasi za juu bila kupata pointi hata mnoja basi ingebidi Vettel asubiri mashindano mengine bila kutangazwa bingwa.

Hata hivyo dua za Button hazikufanikiwa ambapo Mjerumani Vettel aliweza kumaliza wa tatu nyuma ya Fernando Alonzo wa Timu ya magari ya Ferrari.

Akiwa mwenye umri wa miaka 24 na siku 98 days, Vettel ndiye dereva mdogo kwa umri kushinda mashindano haya mfululizo.

Dereva mwingine aliyetazamiwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kushinda mashindano haya Lewis Hamilton wa magari ya McLaren alinusurika panchari ya tairi la gari na vilevile mgongano mdogo na dereva wa Ferrari Felipe Massa na kumaliza wa tano.

Kwa kipindi ilionekana kama Lewis Hamilton angeweza kushinda mbio hizi za Japan, licha ya kuanza katika nafasi ya tatu aliweza kuwapiku madereva wote na kuongoza hadi mkasa wa tairi kupasuka alipolifanyia marekebisho akagongana na dereva wa Ferrari Felipe Massa, ingawa uchunguzi ulionyesha kuwa Hamilton hakukusudia kumgonga Massa.

Hii ni mara nyingine ambapo madereva hawa wanakwaruzana kwenye mashindano. Itakumbukwa kuwa kwenye Mashindano yaliyopita

Mbali na hayo yaliyotokea nje ya mpambano mkali kwenye uwanja wenye kona nyingi wa Suzuka, kijana Vettel anajiweka kwenye orodha ya mabingwa wa magari ikiwemo dereva aliyesifika mno marehemu Ayrton Senna, Alain Prost na Damon Hill waliotunukiwa ubingwa wao kwenye uwanja wa Suzuka wakishinda kwa kufululiza mashindano yanayofuatana.

Punde baada ya kukamilisha mbio hizi Sebastien Vettel hakua na mengi ya kusema ila kuwasifi watu wote waliomsaidia katika kufanikisha safari ndefu ya mashindano ya msimu huu wa mwaka 2011. Bado kuna mbio zilizosalia kwenye ratiba ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na mbio za Korea zitakazofanyika tareh 14 hadi 16 mwezi Oktoba 2011, mbio za India kuanzia tareh 28 na 30 Oktoba, Abu Dhabi tareh 11 na 12 Novemba kabla ya mbio za mwisho kwenye uwanja wa Inter Lagos nchini Brazil zitakazofanyika tareh 25 hadi 27 Novemba.