Bibi Tymoshenko ahukumiwa miaka saba

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ukrain Yulia Tymoshenko amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela, baada ya Jaji kumpata na hatia ya kutumia vibaya madaraka alipokubali na kutiliana saini mapatano ya gesi na Urusi mnamo mwaka 2009.

Haki miliki ya picha
Image caption Bi Tymoshenko na Putin

Akitoa hukumu Jaji alisema kua Bibi Tymoshenko ameisababishia Ukraine kupoteza takriban dola milioni mia mbili, na kumuamuru alipe fedha hizo.

Ndani ya mahakama iliyofurika Bibi Tymoshenko aliitaja kesi nzima kama maonyesho ya kisiasa na kusema kua atakata rufaa.

Akiwa mahakamani Bi Tymoshenko mara kwa mara alimkatiza Jaji aliyekuepo, Rodion Kireyev, wakati akimsomea hukumu, akinadi ''itukuzwe Ukraine'.

Pamoja na kifungo cha miaka saba jela alitozwa faini ya takriban dollar mia mbili.

Alituhumiwa kwa kukiuka mamlaka yake kwa kutia saini mapatano ya gesi na Waziri Mkuu wa Urussi Vladmir Putin mnamo mwaka 2009. Ikumbukwe kuwa mapatano hayo ndiyo yaliyokomesha vita vya gesi baina ya nchi hizo mbili.

Bibi Tymoshenko aliutaja mchakato mzima wa mahakama kama maonyesho ya kisiasa akiongzea kuwa ni kulipiza kisasi kwa sababu alimpinga Rais Viktor Yanukovich

Haki miliki ya picha AP
Image caption Tymoshenko enzi zake

Kesi hiyo ilifuatiliwa kwa karibu huko Marekani na Ulaya, ambako wana balozi wamekubaliana na madai yake.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameonya kua iwapo Bibi Tymoshenko atahukumiwa basi mahusiano ya Ukraine yanaweza kuathirika.

Nje ya jengo la mahakama Kiev ya kati wafuasi wa Bibi Tymoshenko walikusanyika na hofu ilitanda kua wanaweza kuzusha ghasia.