Raia wa Nigeria akiri mashtaka Marekani

Farouk Abdulmutallab Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Farouk Abdulmutallab

Safari ndefu ya Umar Farouk Abdulmutallab kutoka malezi -ya maisha ya anasa hadi --kugeuka kuwa mtu mwenye mawazo ya msimamo mkali katika jiji la London na Yemen na kisha anga za Marekani --imefikia ukiongoni.

Sasa atakaa kifungoni maisha. Jaji Nancy Edmunds alimuuliza Abulmutallab kama anakiri mashtaka na kwa hiyo kusamehe haki yake ya kujitetea mahakamani.

"Ndivyo hivyo kabisa" alisema. Alisomewa shtaka moja baada ya jingine na kwa kila moja alijibu " Nakiri" kwa kutumia silaha za maangamizi; njama ya kuilipua ndege - na kwa jaribio la kuwaua abiria 289 katika ndege iliyokuwa safarini kuelekea ,Detroit.

Aliipenyeza milipuko aliyoificha ndani ya chupi yake hadi katika ndege. Alijaribu kuilipua kwa kutumia sindano ya kuchomea wagonjwa. Miale ya moto ilifuka katika viungo vyake vya siri, lakini hakukuwepo na mlipuko wowote. Na moto ukazimwa na abiria.

Katika taarifa yake fupi kwa mahakama alisema jaribio hilo la kuilipua ndege ni wajibu wake kidini; na liliochochewa na kile alichokieleza mashambulizi ya Marekani dhidi ya Waislamu. Baada ya kukiri kuwa ni mwenye hatia anasubiri tu hukumu rasmi. Na alipoondoka mahakamani Abdulmutallab alinadi " Allahu Akbar" Mungu ni mkubwa.