Upinzani Liberia ulalamikia uchaguzi

Vyama vya upinzani vya Liberia vimewataka wafuasi wao wajumuike kwenye mhadhara leo Jumapili, kupinga uchaguzi wa rais, ambao vinasema umekuwa na udanganyifu.

Haki miliki ya picha REUTERSLucas JacksonFiles

Wapinzani wanasema wana ushahidi kuwa matokeo ya mwanzo yalibadilishwa, wakati wa kuhesabu kura, ili kumpendelea rais wa sasa, Bibi Ellen Johnson Sirleaf.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, James Fromayan, amekanusha tuhuma hizo.

Alisema wasimamizi ndani ya nchi na wa kimataifa walitangaza kuwa uchaguzi uliofanywa Jumaanne, kwamba ulikuwa huru na wa haki.

Matokeo ya hadi sasa, yanaonesha Bibi Ellen Johnson Sirleaf, anaongoza kwa kura chache, lakini hazitoshi kuepuka duru ya pili ya upigaji kura.

Mgombea alioko nafasi ya pili, Winston Tubman, ni kati ya wale wanaodai kumepita ulalamishi kwenye uchaguzi.