Wanawake wa Uganda waokolewa Malaysia

Polisi nchini Malaysia wamesema wamefanikiwa kuvunja mtandao wa biashara ya binadamu uliowaingiza wanawake wa Uganda katika biasahra ya ngono.

Wanawake 21 wengi wao wakiwa na umri wa miaka 20 wameachiliwa kufutaia operesheni maalum ya polisi.

Wanawake hao hurubuniwa baada ya kuahidiwa kuwa wangepatiwa kazi nzuri kabla ya kusafirishwa hadi China.

Baadae safari yao iliishia Malaysia ambako walikuwa watumwa wa ngono.