Mogae ataka wapenzi wa jinsia moja wahalalishwe

Image caption Wakazi wa Botswana

Botswana haina budi kuhalalisha wapenzi wa jinsia moja na biashara ya ukahaba ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya UKIMWI, Rais wa zamani wan chi hiyo Festus Mogae ameiambia BBC.

Bw Mogae, aliyeongoza serikali ya Botswana kuunga mkono Baraza la Aids amesema ilikuwa vigumu kukampeni ngono salama wakati mambo hayo mawili ni si halali.

Ametaka pia mipira ya kiume-kondom zisambazwe magerezani.

Maoni yake hayo yameleta utata wakati wabatswana wahafidhina wanapinga wapenzi wa jinsia moja na ukahaba.

Botswana ni moja nchi zenye idadi ya juu ya watu wenye UKIMWI na virus vya HIV duniani -17% ya idadi yote ya Wabotswana wana virusi vya UKIMWI.

Msemaji wa serikali kuhusu UKIMWI ameiambia BBC kuwa wapenzi wa jinsia moja na makahaba vitaendelea kuwa kinyume cha sheria mpaka hapo serikali itakapofanya mashauriano kwa mapana kuona kana kuna haja ya kufanyia mabadiliko sheria.

Bw Mogae alisema Botswana haiwezi kuchukulia wapenzi wa jinsia moja kundi dogo nchini humo-kama wahalifu.

Sera ya Magereza

"Sielewi mapenzi ya jinsia moja. Sijihusishi nayo," amekiambia kipindi cha BBC Network Africa.

"Navutiwa na wanawake. Sivutiwi na wanaume. Lakini kuna ambao wanvutiwa na wanaume. Hawa ni raia pia."

Alisema serikali inahitaji kubadili sera zake kuhusu watu wanaofanya biashara ya ukahaba kusaidia kupambana na HIV/AIDS

"Kuwalinda wao na wateja wao kuambukizwa, unahitaji kuwasaidia kujilinda wenyewe. Sifikiri kuwakamata kutawasaidia." Alisema Bw Mogae

Alisema kushindwa kwa serikali kuwapa wafungwa kondomu kunafanya hali ya HIV/Aids kuwa mbaya zaidi.

"Iwapo watu wanapelekwa gerezani hawana virusi na wanatoka wakiwa wameambukizwa, ina maana kuwa magereza, vyovyote sheria," alisema Rais huyo wa zamani.

Bw Mogae aliachia uongozi kama Rais mwaka 2008 mwishoni mwa awamu yake ya pili.