Kenya yawarudisha watuhumiwa Uingereza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mpaka wa Kenya

Watu wawili wa Cardiff wamerejeshwa Uingereza baada ya kukamatwa na polisi wa kupambana na Ugaidi nchini Kenya.

Watuhumiwa hao wenye umri wa miaka 18 walikamatwa karibu na mpaka wa Kenya na Somalia wakituhumiwa kuhusika na wapiganaji wa Somalia.

Baba wa Mohamed Mohamed, mwenye asili ya Somalia, aliwajulisha polisi na kusafiri kumtafuta mwanawe akisema ‘amepotoshwa’

Watu hao wawili wanatarajiwa kufika London baadaye Jumatano.

Inatarajiwa kuwa watafanyiwa mahojiano na Polisi wa South Wales baada ya kufika.

Hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa na Kenya dhidi ya Bw Mohamed na Iqbal Shahzad, ambaye ana asili ya Pakistan.

Walirudishwa Jumatano baada ya kuhojiwa na polisi wa kitengo cha kupambana na ugaidi.

Baba mzazi wa raia wa Uingereza mwenye asili ya Kisomali aliambia BBC kuwa alisafiri kwenda Kenya baada ya mwanawe kupotea nyumbani kwao Cardiff.

Abdirhman Haji Abdallah aliuarifu ubalozi wa Uingereza mjini Nairobi pamoja na polisi wa Kenya ba kuwapa picha ya mwanawe.

Vikosi vya usalama vilimakamata kijana wake Mohemed karibu sana mpaka wa Somalia akiwa na rafiki yake.

Bw Abdallah alisema aliungana na mwanawe mjini Nairobi ambako polisi walisema hawatamfungulia mashataka kwani hakuwa amevuka moaka kuingia Somalia, lakini wanengelipeleka shauri lake kwenye Mamlaka za Uingereza.

Tukio la vijana hao wa miaka 18 lilifahamika kuwa hawajulikani walipo kwa zaidi ya wiki lilijadiliwa katika mkutano eneo Grangetown mjini humo Jumapili.

Taarifa ya pamoja kutoka Jumuiya ya Waislamu mjini Cardiff ilisema Jumuiya za Wasomali na Wapakistan na Jumuiya ya Waislamu kwa ujumla wanasubiri kurejea kwao hao wawili.