IGAD yafurahia Kenya kuingia Somalia

Shirika la IGAD limefurahia hatua ya kijeshi ya Kenya dhidi ya Somalia.

Haki miliki ya picha AFP

Shirika hilo limesema linaunga mkono hatua hiyo, pamoja na makubaliano kati ya serikali ya mpito ya Somalia na Kenya, kushirikiana katika operesheni hiyo.

Kenya inasema imechukua hatua hiyo baada ya kuvamiwa mara kwa mara na wapiganaji wa kundi la wapiganaji la al-Shabaab.

Awali juma hili majeshi ya Kenya yaliuteka mji wa Afmadow, kusini mwa Somalia, ulio kituo cha wapiganaji wa al-Shabaab, huku wanajeshi wa serikali ya Somalia wakivamia mji mwengine.