Watano wauwawa Yemen

Wanajeshi wa serikali ya Yemen wamepambana na wanaharakati wa upinzani katika mji mkuu, Sanaa.

Inaarifiwa kuwa watu watano wameuwawa na wengine kadha kujeruhiwa.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema walisikia miripuko katika mji, na kuona moto na moshi ukipaa katika mitaa kadha, ambamo wanajeshi wa upinzani wako.

Siku ya Ijumaa, kura iliyopitishwa kwa kauli moja katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ilimtaka Rais Saleh aondoke madarakani haraka, na badala yake atapewa ahadi kuwa hatofikishwa mahakamani.