Kambi ya al-Shabaab yashambuliwa

Wapiganaji wa al-Shabaab Haki miliki ya picha Reuters

Taarifa kutoka Somalia zinaeleza kuwa kambi moja inayotoa mafunzo kwa wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab, imeshambuliwa na ndege.

Kambi hiyo iko Kismayo - bandari ilioko kusini mwa nchi, ngome ya al-Shabaab.

Mwandishi wa BBC nchini Somalia, anasema ndege zisokuwa na rubani zilihusika na shambulio hilo.

Juma lilopita, wanajeshi wa Kenya walivuka mpaka na kuingia Somalia, wakisema, wakiwasaka wapiganaji wanaoshutumiwa kuwateka nyara wageni kadha nchini kenya.

Na msafara wa kikosi cha Umoja wa Afrika mjini Mogadishu piya umeshambuliwa.