Mweusi achaguliwa upinzani Afrika Kusini

Chama kikuu cha upinzani cha Afrika Kusini, the Democratic Alliance, kwa mara ya kwanza kimemchagua kiongozi mweusi kuwakilisha chama hicho bungeni.

Lindiwe Mazibuko, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 31 ambaye kampeni yake iliungwa mkono na kiongozi wa taifa wa chama hicho, Hellen Zille.

Mwandishi wa BBC aliyopo Cape Town alisema upinzani bado unajaribu kuondosha taswira yake ya kuwa na wafuasi weupe, miaka 17 baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi.

Wakosoaji wameelezea mabadiliko hayo ya uongozi wa bungeni kama unafiki.