Mafuriko mabaya yaifunika Accra

Haki miliki ya picha online
Image caption Mafuriko yaifunika Accra, Ghana

Mafuriko makubwa yamefunika mji mkuu wa Ghana , Accra, na kuua watu tisa, maafisa wanasema.

Mafuriko hayo yameharibu makazi, kukata umeme na kusababisha shule na maduka kufungwa.

Rais John Atta Mills ametembelea amaeneo yaliyoathirika, huku huduma za dharura kuwaokoa watu ambao wamepanda juu ya mapaa ya nyumba kukimbia mafuriko hayo.

Mafuriko mwezi Oktoba nchini Ghana si ya kawaida ambapo msimu wa mvua huanzia mwezi Juni mpaka Agosti, mwandishi waandishi wanasema.

Chombo cha Kitaifa Ghana kinachoshughulikia Majanga (NDMO) kimesema idadi ya watu waliokufa imeongezeka kutoka sita mpaka tisa baada ya miili mitatu kupatikana.

Mwandishi wa habari Samuel Bartells mjini Accra ameiambia BBC kuwa kuendelea kwa mvua siku ya Alhamis, baadhi ya wakazi wana wasiwasi kunaweza kuwa na mafuriko zaidi.

Hata hivyo, mji unarejea katika hali ya kawaida na shule na maduka kufunguliwa, anasema.