Commonwealth itapambana na polio

Viongozi wa Jumuiya ya Commonwealth, wanaokutana mjini Perth, Australia, wameahidi kuzidisha juhudi za kufyeka ugonjwa wa polio.

Haki miliki ya picha Getty

Waziri Mkuu wa Australia, Julia Gillard, alisema nchi yake itatoa msaada wa dola milioni 50 zaidi katika mpango huo wa kimataifa.

Canada na Nigeria piya zimeahidi kutoa fedha zaidi.

Polio imebaki katika nchi nne - India, Pakistan, Nigeria na Afghanistan.

Zote, isipokuwa Afghanistan, ni wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yameshafanya jitihada ya kuondosha polio duniani; na viongozi wa Jumuiya ya Madola, yalenga kuwa ugonjwa huo ufyekwe kabisa ifikapo mwaka wa 2013.