Cameron aiangalia Somalia

David Cameron ametangaza kuwa meli zilizosajiliwa Uingereza zinaweza kuwa na walinzi waliojihami ili kujikinga na maharamia.

Haki miliki ya picha Reuters

Akihojiwa na BBC, Waziri Mkuu wa Uingereza alisema anataka kushughulikia zaidi tishio linalokabili meli katika pwani ya Somalia - ambako meli 49 zilitekwa na maharamia mwaka jana.

Hivi sasa sheria hairuhusu walinzi kubeba silaha kwenye meli za Uingereza, lakini Bwana Cameron alisema anakusudia kubadilisha sheria hiyo:

"Sasa tutasema kwamba meli zilizosajiliwa Uingereza, zitaweza kuwa na walinzi wenye silaha katika meli hizo zikitaka.

Mimi nataka kuhakikisha kuwa maharamia wengi zaidi wanafikishwa mahakamani; na nataka tuitazame zaidi nchi hii ya Somalia iliyoharibika...na vipi tunaweza kujaribu kushughulikia sababu za utekaji nyara, uharamia, kikombozi, na matatizo yote yanayotokana na nchi hii iliyochafuka."