Kagame aona manufaa ya Commonwealth

Rais Paul Kagame wa Rwanda amekanusha tuhuma kuwa serikali yake inakiuka haki za kibinaadamu.

Waandamanaji nje ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola, Perth, Australia, walisema wanapinga Rais Kagame kuhudhuria mkutano huo.

Rwanda iliingia katika Jumuiya ya Madola miaka miwili iliyopita, na Rais Kagame aliiambia BBC sababu ya kufanya hivo:

"Ni kitu kinachovutia.

Kuna kujuana na hiyo inasaidia katika mambo mengi, katika mahitaji mengi ya Rwanda, kama ni uwekezaji, biashara, elimu, au maswala mbalimbali ya maendeleo yetu.

Tunaona kuwa tukiwa katika jumuiya hii ya Commonwealth, ni manufaa makubwa."