Mmarekani alishambulia Mogadisu

Kundi la wapiganaji wa Somalia, al-Shabaab, linasema kuwa Mmarekani mwenye asili ya Somalia alikuwa kati ya watu waliojitolea mhanga, walioshambulia askari wa Umoja wa Afrika mjini Mogadishu, Jumamosi.

Haki miliki ya picha AFP

Video iliyotolewa na al-Shabaab inaonesha kijana akizungumza kwa lafdhi ya Kimarekani - Abdisalan Taqabalahullaah - ambaye anasema alihamia Marekani alipokuwa mtoto wa miaka miwili.

Anasema alirudi Somalia kumtafuta Mungu.

Walioshuhudia shambulio la jana, wanasema watu kama 20 waliuwawa - wakiwemo wanajeshi wa AU na wapiganaji wa al-Shabaab.