Mkuu wa tume ya uchaguzi Liberia ajiuzulu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wananchi wa Liberia wakimsikiliza mgombea

Mgombea wa Upinzani katika duru ya pili ya uchaguzi wiki ijayo nchini Liberia, Winston Tubman, ameukaribisha uamuzi wa mkuu wa tume ya uchaguzi kujiuzulu kutokana na tuhuma za udanganyifu.

Bw Tubman, mwanadiplomasia wa zamani wa Umoja wa Mataifa amesema chama chake kitaamua baadaye Jumatatu iwapo itasitisha mpango wake wa mgomo kupiga kura Novemba 8.

James Fromayan amesema anajiuzulu kwa sababu hataki kuwa kikwazo wakati wa duru ya pili ya uchaguzi.

Bw Tubman anachuana na mshindi wa tuzo ya Nobel Ellen Johnson-Sirleaf.

Ni mwanamke wa kwanza barani Afrika kuchaguliwa Rais baada ya uchaguzi wa 2005 uliomaliza miaka 14 vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia.

Chama cha Bw Tubman cha Congress for Democratic Change (CDC) kilidai Bw Fromayan ajiuzulu kikisema kisingeshiriki katika duru ya pili ya uchaguzi iwapo angebakia katika nafasi yake.

Kilituhumu kusambaa kwa udanganyifu katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo mwezi uliopita.

"Tulipeleka ushahidi wa karatasi za uchaguzi zenye picha zilizokosewa na na wafanyakazi wa Tume," meneja wa kampeni wa CDC George Solo ameliambia Shirika la Habari la AFP.

"Tulipeleka pia karatsi za kura zikiwa zimejharabiwa na namba zao zimebadilishwa. Watu wa wazima walitaka kupiga kwa watu Fulani lakini wafanyakazi wa Tume ya uchaguzi kuwasaidia

Kabla ya kujiuzulu Bw Fromayan alikanusha tuhuma hizo za udanganyifu.