Huwezi kusikiliza tena

Kauli ya Cameron yaleta mtafaruku Afrika

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, siku za hivi karibuni aliwaambia wanachama wa jumuiya ya madola mwishoni mwa wiki katika kikao chao huko Australia, kuwa huenda akakatiza misaada kadhaa kwa nchi ambazo haziruhusu mapenzi ya watu wa jinsia moja, suala hilo limechukuliwa kwa hisia tofauti sana hasa barani Afrika.

Mjadala huu unaangazia suala hilo, na wachangiaji ni

1) Manoah Esipisu- Msemaji wa jumuiya ya madola- London.

2) Hellen Kijo-Bisimba- Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu LHRC - Tanzania

3) Aggrey Awori- Aliyekuwa waziri wa habari na teknolojia ya mitandao- Uganda

4) Kaiza Buberwa- Mwanasheria- Tanzania