Huwezi kusikiliza tena

Meli yatoa huduma za afya Tanzania

Ukosefu wa huduma za afya katika maeneo mengi ya Afrika ni jambo lililozoeleka, lakini kwa raia mmoja wa Marekani yaliyomkuta akiwa katika likizo ya mapumziko huko Ziwa Tanganyika yanakaribia kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu maeneo hayo.

Miaka michache iliyopita Dr. Amy Lehman, aliugua ghafla baada ya boti aliyokuwa akisafiria kukumbwa na dhoruba kali. Aliporejea Marekani akaamua kuanzisha mpango wa kuchangisha fedha za kununulia meli itakayofanyiwa marekebisho na kuwa hospitali itakayohudumia watu wa kando kando ya Ziwa Tanganyika.

Hassan Mhelela anasimulia zaidi kutoka huko alikofanya ziara hivi karibuni.