Huwezi kusikiliza tena

Maonyesho ya ubunifu wa mavazi Tanzania

Mashabiki wa maswala ya mitindo na mavazi nchini Tanzania wamekuwa wakiburudika na tamasha la maonyesho ya mavazi yajulikano kama Swahili Fashion Week mjini Dar es salaam.

Maonyesho hayo yaliyoanzishwa miaka minne iliyopita, yamevutia wabunifu kutoka Afrika mashariki na kati. Jumla ya wabunifu 50 wa mavazi na mitindo na vilevile wanamitindo walikusanyika pamoja kuonyesha mavazi yao.

Mwandishi wetu Tulanana Bohela alihudhuria tamasha hilo.