Huwezi kusikiliza tena

Utalii wakuza uchumi Tanzania

Wakazi walioko kando kando ya Ziwa Tanganyika upande wa Tanzania kwa miaka mingi wamekuwa wakitegemea zaidi shughuli za uvuvi, lakini sasa utalii umeanza kukuza uchumi na kutoa ajira kwa wakazi hao.

Safari ya kufika Ziwa Tanganyika kutoka sehemu kama Dar Es Salaam inataka ujasiri kutokana na umbali na vile vile barabara mbovu yenye vumbi kali; hata hivyo ufikapo ziwani huwezi kujutia uzuri wa mandhari na maji safi na shughuli mbali mbali za kitalii ikiwa ni pamoja na kupiga mbizi au makasia.

Mwandishi wetu Hassan Mhelela alifika katika kijiji cha Kipili mkoani Rukwa na kutuandalia taarifa hii.